×

Kamwe Atamba na Yanga “Tunataka Kubeba Makombe Hadi 2030” – Video

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe, ametangaza kwa kujiamini kuwa malengo ya klabu hiyo ni kuendelea kutawala soka la Tanzania na Afrika Mashariki hadi mwaka 2030, wakilenga kubeba makombe kila msimu.

Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa mataji matano ambayo Yanga SC imeyashinda katika msimu wa 2024/2025, Kamwe amesema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya mipango madhubuti, umoja wa viongozi, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki.

“Hili ni taji letu la nne mfululizo kwenye Ligi Kuu NBC Premier League, na tumeongeza mengine manne ndani ya msimu mmoja. Lengo letu ni moja tu – kubeba makombe hadi 2030!” alisema Kamwe mbele ya wanahabari na mashabiki wa klabu hiyo.