×

Pichaz: Hasira za Yanga… Yantwanga Kiluvya United 6-1

MABINGWA watetezi wa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara, Young African Sc (Yanga) wameendeleza hasira zao kwa kuitwanga klabu ya Kiluvya United kwa mabao 6-1 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ulioigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kusisimua, Kiluvya walianza kwa kasi huku wakigongeana pasi zakaribu karibu kumbe Yanga walikuwa wakiwasikilizia tu.

Hali ilibadilika kunako dakika ya 10 baada ya Yanga kujipatia bao la kwanza kupitia kwa Geofrey Mwashiuya.

Chirwa na Kaseke wakipongezana
Chirwa na Kaseke wakipongezana

Dakika 12 baadaye mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akafumania nyavu za Kiluvya United kunako dakika ya 22  na kuiandikia Yanga bao la 2 huku.

Dakika ya 40, Edgar Charles akaiandikia Kiluvya bao la kufutia machozi.

Chirwa akiwa na uchu wa mabao akafumania tena nyavu za Kiluvya United kunako dakika ya 45 na kwenda mapumziko Yanga wakiongoza kwa bao 3-1.

Kipindi cha pili Yanga hawakuridhika na bao hizo 3, wakakaza tena.

Yanga hawajatosheka, Chirwa akarudi tena dakika ya 71 na kuandika bao la 4.

Dakika ya 76, Juma Mahadhi anaiandikia Yanga bao la 5.

Chirwa huyo huyo akamaliza mchezo kwa kuandika bao la 6 kunako dakika ya 87.

Kikosi cha Yanga First Eleven na sub
Kocha Hans Van Pluijm
Aliyekuwa Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm (kulia) akizungumza na mmoja wa watazamaji uwanjani hapo.

Hadi mchezo unamalizika, Yanga 6-1 Kiluvya United.

Kikosi cha Kiluvya United
Kikosi cha Kiluvya United

Chirwa ameonekana staa kwa mchezo wa leo huku peke yake akifunga bao 5 na kuondoka na mpira wa zawadi.

Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Yanga.

PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS