×

Mgombea Urais wa CUF, Gombo Samandito, Akabidhiwa Fomu na NEC

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 13 Agosti, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi),  Gombo Samandito Gombo. Hafla hiyo imefanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma. Gombo aliambatana na mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya Chama hicho, Mhe. Husna Mohamed Abdalla.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, Agosti 13, 2025, alikakabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mgombea wa Chama cha The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi), Gombo Samandito Gombo.

Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za Tume, zilizopo Njedengwa, jijini Dodoma.

Gombo aliambatana na mgombea mwenza wa kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya CUF, Mhe. Husna Mohamed Abdalla.