×

Watanzania Wanufaika Na Ujio  Unaotarajiwa Kuzinduliwa Ivi Karibuni Ya Bluu Inatawala 

WATANZANIA zaidi ya 145 wamenufaika na ujio unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya Blue inatawala ambapo wamepatiwa huduma mbalimbali ikiwemo kulipiwa huduma za matibabu na kuongezewa Mitaji ya biashara zao.

Akiongea Leo Oktoba 21 Jijini Dar es salaam mwakilishi wa taasisi hiyo Masihi ‘Mr Bluu’ amesema ujio huo mpya imeanza Kwa kutoa huduma Kwa jamii ikiwa ni sehemu ya uanzishi wake kabla ya kutangazwa rasmi.

Amesema huduma hizo wamefanikiwa kuwapunguzia madeni wagonjwa zaidi ya 40 katika Hospitali ya Mwananyamala na Amana na kuwaongezea Mitaji Wajasiliamali zaidi ya 30 wakike na wakiume

Lakini pia watawalipia nauli abiria zaidi ya 75 , yote haya wamefanya ikiwa sehemu ya kujitolea Kwa jamii wakati wakizindua Bluu inatawala .

“Kwa kiwango kikubwa tumesaidia wakina mama kwakuwa wao ndiyo wenye changamoto kubwa, wengine wameachwa na Bado wanalea familia” alisema Mr Blue.

Mfanyabiashara wa kariakoo Ester Paulo amewataka wakina mama kufanya biashara Kwa bidii, Ili misaada kama hivyo inavyokuja waweze kuongezea zaidi.

Amesema wamesaidiwa fedha kidogo nakuwashukuru, huku aliomba Serikali kuweka mazingira mazuri Kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya Majengo.

Mwisho

Leave a Comment