
Dar es Salaam, Oktoba 23, 2025: Sanlam na Allianz, makampuni mashuhuri katika sekta ya bima ambao waliungana pamoja mwaka 2023 kuunda kampuni kubwa zaidi barani Afrika ya huduma za kifedha zisizo za benki, SanlamAllianz, wamezindua rasmi chapa ya SanlamAllianz nchini Tanzania leo.
Akizungumza wakati Uzinduzi huo, uliofanyika jijini Dar-es-Salaam Mgeni rasmi Dr.Baghayo A Saqware kamishina wa bima Tanzania amepongeza hatuna hiyo ambayo itawezesha utekelezaji ambao utakuwa na ubora Katika utoaji huduma za Bima Nchini.

“Uanzishwaji wa SanlamAllianz General Insurance Tanzania Ltd na SanlamAllianz Life Insurance Tanzania Ltd unaonyesha utekelezaji endelevu wa uanzishaji wa chapa hii mpya katika nchi mbalimbali barani Afrika,”amesema Dr.Saqware.
Jaideep Goel, Mkurugenzi Mtendaji wa SanlamAllianz General Insurance, amesema Kampuni yao inalenga kutumia utaalamu wake wa kimataifa wa pan-Afrika kufungua fursa za ukuaji katika uchumi wenye uwezo mkubwa barani Afrika. Ikiongozwa na lengo lake la kuwezesha vizazi kujiamini kifedha, kuwa na usalama na kustawi, kampuni hii inataka kupanua upatikanaji wa huduma za fedha na kuimarisha ujumuishaji wa fedha kwa kutoa suluhisho bunifu zinazounda thamani kwa wadau wote.
“Uzinduzi wa chapa ya Sanla
mAllianz Tanzania ni hatua muhimu kwa ushirikiano wetu pamoja na sekta ya huduma za fedha nchini hii inaonyesha mkakati wetu wa kutumia utaalamu wetu katika masoko yanayokua, kuunda biashara zinazoongoza katika uchumi tunaoufanyia kazi, na pia inaunga mkono dhamira yetu ya kuwezesha watu wengi zaidi kupata huduma za fedha.
mAllianz Tanzania ni hatua muhimu kwa ushirikiano wetu pamoja na sekta ya huduma za fedha nchini hii inaonyesha mkakati wetu wa kutumia utaalamu wetu katika masoko yanayokua, kuunda biashara zinazoongoza katika uchumi tunaoufanyia kazi, na pia inaunga mkono dhamira yetu ya kuwezesha watu wengi zaidi kupata huduma za fedha.
Kupitia ushirikiano huu, tunaweza pia kuunganisha nguvu na uwezo wa kimataifa wa Sanlam na Allianz kwa fursa kubwa za usambazaji, utaalamu na ushirikiano katika mawasiliano na bancassurance, tuna uhakika wateja wetu watanufaika na suluhisho bunifu za mahitaji yao.”
“Kipaumbele chetu ni kutoa suluhisho za bima za jumla zenye kuaminika na za viwango vya kimataifa ambazo zinahifadhi kile kinachowajali zaidi watu na biashara nchini Tanzania. Uzinduzi huu si tu kuhusu chapa mpya; ni kuimarisha ahadi yetu ya kusimama na wateja wetu katika kila hatua ya maisha na kila changamoto wanayokabiliana nayo.”amesema.Bw.Goel.
