
Mtoto wa staa maarufu wa filamu nchini Tanzania, Kajala Masanja, na mtayarishaji nguli wa muziki P Funk Majani, Paulah Kajala (@therealpaulahkajala), amefunguka kuhusu maisha yake ya sasa na kuzungumzia tetesi za ndoa yake na nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Marioo.
Akizungumza hivi karibuni, Paulah amesema kwa sasa hana muda wa kujibu maswali kuhusu ndoa, na kwamba mambo hayo ni vyema wakaulizwa upande wa Marioo.
“Masuala ya ndoa muulizeni mzazi mwenzangu, mimi kwa sasa nimeelekeza nguvu zangu kwenye kutafuta fedha,” alisema Paulah kwa msisitizo.
Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni, huku mashabiki wake wengi wakimpongeza kwa kuzingatia kazi na kujitegemea katika umri mdogo, wakati wengine wakionyesha hamu ya kujua mustakabali wa uhusiano wake na Marioo.
Paulah, ambaye ni miongoni mwa vijana maarufu zaidi kwenye mitandao ya kijamii, amekuwa akihusishwa mara kwa mara na mafanikio ya muziki wa Marioo na maisha ya kifahari wanayoishi, lakini anasema anapenda kutengeneza jina na mafanikio yake binafsi.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment na subscribe ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli, umahiri na uhakika.