
Taasisi ya The Same Qualities Foundation inayotoa matibabu bure ya watoto wenye mdomo wazi (sungura) yaandaa marathon itakayo fanyika Tanzania Zanzibar.
Watoto hao ni wale wenye umri chini ya miaka mitano kwa lengo likiwa ni kuwarudishia furaha watoto hao na kuishi kama wengine.
Taasisi hiyo ina miaka 11 ya utendaji kazi hiyo ambapo mwaka huu zitafanyika Desemba 21 kisiwani Zanzibar.
Lengo la marathoni hiyo ni kuchangisha fedha za matibabu ya watoto hao ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni shilingi 8,000,000 (milioni nane).
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Balozi wa SQF, Juma Ikangaa alisema katika kuwasaidia watoto hao kila mtanzania atachangia kiasi cha Shilingi 35,000 ikiwa ni gharama ya kiingilio cha kujisajili kushiriki mbio hizo.
“Ninawaomba sana watanzania wenzangu kuona hili jambo kama jambo letu mtoto wa mwenzio ni wako na afya ndio kila kitu utakapo changia na itasaidia kiasi kikubwa sana matibabu na furaha kwa watoto hao’alisema.
Alisema tangu kuanza kwa SQF miaka 11 ,ndani ya miaka saba ya mbio hizi tayari watoto 2543 wamefanyiwa upasuaji katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Anasema SQF inatarajia kumtibu kila mtoto atakayefika kwani gharama za matibabu ni kubwa mtu wa kawaida kuzimudu ni ngumu.
Aliongezea endapo utachangia inatumika kumrudishia faraja mtanzania ambaye atasaidia taifa kwa baadae.
“Watoto ni wengi wenye matatizo hayo ya mdomo (sungura) lakini wazazi wanawaficha kutokana na gharama za matibabu yake yaliyovyokuwa juu’alieleza Ikangaa.