The House of Social Media
gunners X

Rais Dkt. Samia Atunuku Kamisheni Kwa Maafisa Wanafunzi Wa JWTZ, Monduli (Picha +Video)

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi kuwa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika cheo cha Luteni Usu kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha tarehe 22 Novemba, 2025.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan akitoa zawadi kwa Maafisa Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi wakati wa Mafunzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anongoza hafla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka makundi mawili ya mafunzo: kundi la 06/22 – BMS na kundi la 72/24 – Regular. Hafla hiyo imefanyika tarehe 22 Novemba 2025, katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (Tanzania Military Academy – TMA) Monduli, mkoani Arusha.

Katika tukio hilo muhimu la kijeshi, Rais Samia atawapandisha vyeo maafisa wanafunzi na kuwatunuku Kamisheni kama ishara ya kuhitimu mafunzo yao rasmi ya kijeshi, hatua inayowatambulisha kama maafisa kamili wa JWTZ. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, makamanda wa JWTZ, familia za wahitimu, pamoja na wageni waalikwa.

Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba, 2025.
Matukio mbalimbali wakati wa sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha tarehe 22 Novemba, 2025.

Leave A Reply