Yanga Yakaribia Kumnasa Straika wa Cameroon Kuchukua nafasi ya Andy Boyel

YANGA wanahusishwa katika usajili wa mshambuliaji raia wa Cameroon, Taddeus Nkeng Fomakwang anayekipiga Klabu ya Carabobo FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Venezuela katika usajili wa dirisha dogo msimu huu.
Kwa mujibu wa chanzo kutoka ndani ya Yanga, Mcameroon anakuja kuchukua nafasi ya mshambuliaji, Andy Boyel ambaye inaelezwa ameshindwa kumshawishi kocha Pedro Goncalves.
Inaelezwa kuwa mshambuliaji huyo yupo katika mazungumzo ya mwisho na Viongozi wa Yanga kwa ajili ya kukamilisha dili hilo ili aje kukiongezea nguvu kikosi hicho msimu huu.
STORI NA WILBERT MOLAND, GPL


