The House of Social Media
gunners X

Waziri Kikwete Asisitiza Uweledi na Uwajibikaji kwa Wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma

0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete ameielekeza Bodi ya Ushauri na Menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kujikita zaidi katika kufundisha kozi zitakazoenda kutatua changamoto za wahitimu na wananchi kwa ujumla.

Waziri Kikwete ametoa maelekezo hayo Novemba 28, 2025 kabla ya kuwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya 42 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kikwete amesema, Watanzania wanahitaji kupata elimu ya kuwasaidia katika maisha yao na sio ya kukaa na vyeti ndani. “Naielekeza Bodi na Menejimenti kuhakikisha Kozi tunazoanzisha zinaleta majawabu ya changamoto za Watanzania,” Mhe. Kikwete amesisitiza.

Mhe. Kikwete amesema anayo maswali ya msingi ya kujiuliza, akitolea mfano wa Kozi ya Makatibu Mahususi, je Kozi zilizotolewa kwa watumishi hawa zamani zinafanana na zinazotolewa sasa? Tumeshuhudia uvunjifu wa maadili kwa watumishi. Ni wajibu wetu kuhakikisha watumishi wanakuwa na uadilifu, tutengeneze Utumishi wa Umma wenye weledi. Je watumishi wa umma bado ni wazalendo? Ni majibu yanayopatikana kwa Menejimenti na Bodi ya Chuo hiki. Tuangalie Mitaala ili ijibu maswali yangu,” amesisitiza.

Aidha, ametoa wito kwa Wahitimu kuendelea kujifunza hata baada ya kuhitimu, kwani dunia ya leo inahitaji kujifunza maisha yote ili kuendelea kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yanayobadilika kila uchwao.

“Nawasihi mjiepushe na vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu taswira yenu na ya Utumishi wa Umma, kama vile rushwa, uzembe, ubaguzi, matumizi mabaya ya madaraka na kutowajibika. Badala yake, muwe mfano wa kuigwa katika weledi, uwajibikaji, uadilifu na kujituma kazini,” ameongeza

“Leo mmehitimu, na baadhi yenu kesho mnatarajiwa kuwa viongozi na watendaji katika sekta mbalimbali. Taifa linawategemea hivyo mtakapopata fursa ya kuajiriwa mkawe mabalozi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kwa kufanya kazi kwa kuzingatia.

WAZIRI MKUU MWIGULU kwa UKALI AFICHUA MCHEZO MCHAFU UNAOENDELEA – “INAKASIRISHA – WANAGAWA WATU”..

Leave A Reply