Waziri Ulega Akutana na RC Makalla Kujadili Kasi ya Miradi ya Miundombinu Jijini Arusha

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huyo kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa Miundombinu jijini Arusha.
Waziri Ulega amemuahidi Mkuu wa Mkoa huyo kuendelea kusimamia na kutoa msukumo wa usimikaji wa taa katika barabara za Arusha, upanuzi wa barabara ya Arusha-Kisongo na Arusha-Moshi ambayo itapunguza foleni na kurahisisha usafiri kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA), hasa katika kuelekea maandalizi ya AFCON 2027.
Aidha, Ulega ametoa wito kwa watanzania kuilinda miundombinu ya barabara, taa na samani za barabara zinazowekwa kwani inagharimu fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kutekeleza miradi mingine.


