×

Benki ya Azania Yaja na Huduma Muhimu Kuwanufaisha Wanavyuo na Waajiriwa

Dar es Salaam, 2 Desemba 2025: Katika kuendeleza juhudi za serikali katika kubotesha Sekta ya elimu na kutoa unafuu kwa wafanyakazi, Benki ya Azania leo imezindua huduma mbili zitakazowanufaisha wanafunzi wa elimu ya Juu pamoja na watumishi wa Umma na wale wa Sekta Binafsi.

 

Ambao waajiri wao Wana mikataba na Benki ya Azania.

Huduma hizo zinajulikana kama ‘Boom Advance’ na ‘Salary Advance.’

Kwa upande wa Boom Advance huduma hii inalenga wanafunzi wa elimu ya Juu wanaopata mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya elimu ya Juu (HESLB).

Kupitia huduma huu wanavyuo hawatalazimika kusubiri hadi mikopo yao iingie kwenye akaunti.

Bali wataweza kupata mikopo wa muda wenye masharti nafuu ili waweze kujikimu Wakati wakisubiri fedha kutoka HESLB.

Huduma ya pili ni Salary Advance ambayo imelenga watumishi.

Huduma hii itamuwezesha mwajiriwa kupata sehemu ya mshahara wake kabla ya tarehe ya kawaida ya kuingiziwa mshahara.

Kupitia mkopo huu wa muda mfupi mwajiriwa ataweza kukidhi mahitaji yake muhimu ya kufedha Wakati akisubiri mshahara kuingia mwisho wa mwezi.

Mkopo huu hurudishwa mara moja mshahara unapoingia kwa riba nafuu ya 5% tu.

Mteja ataweza kukopa hadi nusu ya mshahara wake wa mwezi.

Katika kuendeleza mageuzi ya kidigitali ndani ya Benki ya Azania huduma hizi zote zinapatikana kupitia simu yako ya  mkononi kwa kubofya *150*75# kupitia Azania Bank Mobile App au Internet Banking.

Akizungumza katika uzinduzi huo Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Masoko, Bi Elizabeth Nyattega amesema kuwa benki hiyo imeendelea kufanya maboresho makubwa katika huduma zake kiasi cha kutunukiwa Tuzo ya Ubora Kidijitali, Afrika Mashariki 2025 katika tuzo za Africa Bank Award 4.0 2025.

Leave a Comment