Mixx Yazindua Kampeni Kubwa ya Mwisho wa Mwaka

Leo, Mixx, imezindua kampeni kubwa ya mwisho wa mwaka – Magift ya Mixx Pesa- ikiwa ni shukrani kwa wateja wanaoendelea kuichagua Mixx, kila siku.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha alisema
“Katika msimu huu wa sikukuu wenye mahitaji mengi, Mixx inakuja na zawadi nono kupitia kila muamala, ikiwemo milioni 1 kila siku, milioni 5 kila wiki, ushindi wa milioni 10 MixxMas, na mwaka mpya na Jackpot ya milioni 50 mwishoni mwa kampeni.
Kampeni hii ni uthibitisho wa jinsi tunavyothamini uaminifu wa wateja wetu na dhamira ya kuendelea kubuni huduma rahisi, nafuu na zinazowawezesha katika malipo, akiba na mahitaji yote ya kifedha. Tunawaalika wateja wote kutumia huduma zetu za wakala, Mixx Super App au *150*01# ili kupata nafasi ya kushinda na kuufunga mwaka kwa nguvu kupitia “Magift ya Mixx Pesa”

