The House of Social Media
gunners X

Mahakama ya Kisutu Yawaachilia Huru Jennifer Jovin ‘Niffer’ na Mika Chavala

0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachilia huru mfanyabiashara Jennifer Jovin, maarufu kama Niffer (26), na Mika Chavala (32), baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuondoa mashtaka dhidi yao.

Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatano Desemba 3, 2025, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya, kufuatia kuwasilishwa kwa hati ya Nolle Prosequi taarifa rasmi ya DPP ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka kwa mujibu wa kifungu cha 92(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, marejeo ya 2023.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

Leave A Reply