The House of Social Media
gunners X

Majizzo Awaombea Msamaha Wasanii Baada ya Mashabiki Kususia Kazi Zao

0
Mkurugenzi wa Efm na TVE

Mkurugenzi wa Efm na TVE, amejitokeza hadharani kuomba msamaha kwa wasanii wa Tanzania baada ya mashabiki kutangaza kususia kazi zao.

Sababu ya hatua hiyo ni kuhusiana na malalamiko ya mashabiki kwamba baadhi ya wasanii hawajapaza sauti yao kwa serikali juu ya changamoto wanazopitia wananchi, jambo lililozua hisia mseto mitandaoni.

Majizzo, kupitia taarifa yake, alisema kwamba lengo lake ni kuunga mkono wasanii na kuhakikisha wanahusiana vyema na mashabiki, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wasanii na jamii katika kuibua mijadala yenye manufaa kwa taifa.

Wasanii hao wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo la mashabiki, baadhi wakisema hawana sauti ya kutosha kulalamikia hali mbaya ya kijamii au kuibua masuala muhimu yanayowakabili wananchi. Tukio hili limeonesha wazi mgogoro wa mahusiano kati ya wasanii na mashabiki.

Kwa upande wake, Majizzo ametoa wito kwa mashabiki kurejesha imani kwa wasanii, na kuacha hatua za kuwakataa au kususia kazi zao, akisisitiza kuwa kila upande unapaswa kushirikiana kwa manufaa ya jamii.

Kauli Kamili ya Majizzo

“Natoa pole kwa yote yaliyotukuta baada ya Uchaguzi wa Oktoba 29, kubwa zaidi wale waliopata misiba. Natambua maumivu yenu, Mungu mwenyewe awe mfariji kwenu. Pole kwetu sote.

Nimejiridhisha kwamba huu ni wakati sahihi kuja kwenu kuzungumza, lengo langu mahsusi ikiwa sekta ya muziki na hasara tunayotengeneza kwa Watanzania wanyonge.

Ni kweli wasanii wwanaathirika, lakini athari kubwa zaidi ipo kwa kundi kubwa linalotegemea hizo kazi za sanaa: dancers, wapiga vyombo, makeup artists, wauza nguo na wengine wengi. Familia zao vipi?

Moja vilio ambavyo tunalia wote ni kilio cha ukosefu wa ajira, hivyo tusizipige teke hizi ajira kwenye kiwanda cha muziki kwa sababu kuna watu wachache wametukasirisha.

Msamaha ninaoomba ni kwa sababu nafahamu kuna mahali wadogo zangu hawa walipitiliza na sio kwa sababu walifanya kampeni. Huu muziki ni wenu. Mkiumiza tasnia, mnaumiza maelfu ya ajira. Naomba radhi, na ikiwapendeza naomba muendelee kuupa nguvu muziki wenu.”

APATA UVIMBE TUMBONI WAAMIA SEHEMU ya SIRI – YAGUNDULIKA KANSA – ATAKIWA KUCHANWA TUMBO AISHI…

Leave A Reply