Nmb Yakabidhi Vifaa Tiba Vyenye Thamani ya Mil 15 Kituo Cha Afya Makole Dodoma

Msaada huo unalenga kusaidia kituo hicho kuboresha utoaji wa huduma za afya na kukidhi mahitaji ya wananchi wanaopata huduma katika eneo la Makole na maeneo jirani.
Vifaa hivyo vilipokelewa na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole, Dkt. Revocatus Kitena. Uwakilishi wa Benki katika hafla hiyo uliongozwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango, akiambatana na baadhi ya Mameneja wa Matawi wa NMB Kanda ya Kati.




