Inspector Haroun atoa nyimbo mpya AI na Maisha Ndo Haya, Afunguka Mapaya – Video

Msanii wa Bongo Flava, Inspector Haroun, amesema alimshirikisha msanii Ibraah katika wimbo wake Final Sub kutokana na nidhamu, heshima na kujituma kwake katika kazi ya muziki.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo, Inspector Haroun amesema Ibraah ana kiu ya kubarikiwa na wasanii wakubwa, hali inayomfanya kuwa mnyenyekevu na mwenye heshima, huku akimchukulia kama kaka yake, jambo lililomvutia na kumpa imani ya kufanya naye kazi.
Wakati huo huo, Inspector Haroun ameendelea kuwapa burudani mashabiki wake kwa kuachia nyimbo mbili mpya zinazokwenda kwa majina ya AI na Maisha ndo haya. Nyimbo hizo tayari zinapatikana katika majukwaa yote ya kusikiliza na kutazama muziki.

