The House of Social Media
gunners X

Mchango wa GGM Waibua Tumaini kwa Watoto 420 Wenye Matatizo ya Moyo

0

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), inahitaji shilingi bilioni 1.6 kwaajili ya kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto 420 wanaougua maradhi ya moyo ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu yao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Heart Team Foundation Africa, Dk Naiz Majani, aliyezungumza kwa niaba ya JKCI wakati wa hafa ya kuupongeza mgodi wa madini wa Geita Gold Mine (GGM) kwa kusaidia upasuaji wa watoto 14 wanaougua moyo katika taasisi hiyo.

Alisema HTFA kwa kushirikiana na JKCI mwaka jana walifanya harambee kukusanya fedha za matibabu kwa wagonjwa wa moyo ambapo GGM ni miongoni mwa wadau wengi waliotoa fedha kugharamia matibabu hayo.

“Tulipowaomba GGM walichangia shilingi milioni 56, matibabu ya moyo ni gharama kubwa sana duniani kote na kwa hapa Tanzania  asilimia 70 ya matibabu hayo gharama inakuwa kwa serikali na asilimia 30 kwa wazazi lakini bado asilimia 30 ni kubwa sana kwa mtanzania wa kawaida,” alisema

Alisema kwa mwaka 2025 HTAF ilifanikiwa kusaidia watoto 303 kupata matibabu ya moyo kwa upasuaji wa moyo na asilimia tano wamesaidiwa na GGM na maendeleo yao ni mazuri kwa kiwango cha asilimia 95.


Leave A Reply