
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ametoa kauli nzito jana wakati wa hafla ya kukabidhiwa ofisi kutoka kwa mtangulizi wake Profesa Palamagamba Kabudi, akieleza mwelekeo wake wa uongozi na matarajio kwa watumishi wa wizara hiyo.

Mambo 10 Aliyoyasema Makonda jana
1. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda ametaja mambo kumbi wakati anakabidhiwa ofisi hiyo na Profesa Palamagamba Kabudi jana, amesema kwamba Mtumishi wa Wizara ya Habari, Ukivaa Vibaya utakomea getini.
2. Ndani ya Mwaka mmoja hii itakuwa Wizara ambayo itawavuti hata watumishi wa Wizara zingine ikiwemo Wizara ya fedha.
3. Wale Wakuu wa Idara na Vitengo ambao hawajatekeleza baadhi ya mambo ambayo walikubaliana, waende na maelezo kwa nini waendelee kuongoza hivyo Vitengo.
4. Mhe Waziri atamuomba Mhe Rais Bil 2 kwa ajili ya “Content Creators” ili kuwasaidia katika shughuli zao za uandaaji maudhui.
5. “Maafisa habari wa Wilaya wanatakiwa kuhakikisha wanaripoti changamoto kabla wananchi hawajazipeleka kwa Waandishi wa habari” Kauli ya Waziri Makonda.
6. “Tofauti ya yangu na Mhe. Kabudi ni Speed. Yeye alikuwa anatumia busara, anaangalia Jambo kisha anafananisha ya miaka ya 70 ilikuwaje. Kwangu ni spidi muda wa kutafuta rekodi sina” Amesema Makonda
7. Waziri Makonda anasema kwamba watendaji wa Wizara hiyo wakae vizuri kwenye viti vyao na waenee Kisha wakaze mikanda.
8. Watu wa mambo ya Utamaduni wajipange kwa sababu wao wamekuwa wanaangalia tu kutoa vibali wapate hela, na hakuna kazi nyingine inayofanyika. Amesema Makonda.
9. Makonda amesema kwamba rekodi yake inajulikana, hana tabia ya kucheka wakati moyoni amenuna, na hana tabia ya kununa moyoni wakati usoni anacheka. Anachotaka ni kazi kazi.
10. Kwenye kuvaa vizuri anasema inatoka na Wizara hiyo kuwa ndio inayosimamia mambo mengi yanyohusu watu Maarufu, kwa hiyo muonekano na kukaa kijanja kwa watumishi ni jambo la muhimu.
Stori na Elvan Stambuli, Global
<iframe width=”830″ height=”455″ src=”https://www.youtube.com/embed/e11lDb4OSG4″ title=”ROSE MUHANDO AFICHUA ANAVYODHULUMIWA PESA KWENYE NYIMBO ZAKE – AMLILIA MAKONDA AINGILIE KATI…” frameborder=”0″ allow=”accelerometer; autoplay; clipboard-write; encrypted-media; gyroscope; picture-in-picture; web-share” referrerpolicy=”strict-origin-when-cross-origin” allowfullscreen></iframe>

