Video: Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu Yapangwa Kuendelea Februari 2026

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA Taifa, Gaston Galubindi, kesi ya uhaini Namba 19605/2025 inayomkabili Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, imepangwa kuendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kuanzia Februari 09 hadi Machi 06, 2026.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa Novemba 12, 2025, kesi hiyo iliahirishwa kwa muda usiojulikana baada ya Mahakama kueleza kuwa ingetangaza tarehe mpya ya kuendelea na usikilizaji. Hii ilitokea licha ya notisi ya awali kuonesha kuwa siku hiyo ingekuwa ni mwisho wa mchakato wa kusikiliza kesi hiyo.

