×

Trump Akabidhiwa Tuzo ya Amani ya Nobel na Kiongozi wa Upinzani wa Venezuela

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kutoka Venezuela amemkabidhi Rais wa Marekani, Donald Trump, tuzo yake, katika mkutano wa faragha uliofanyika Ikulu ya White House siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa kauli ya kiongozi wa upinzani wa Venezuela, María Corina Machado.

Akizungumza baada ya mkutano huo, Machado alisema tukio hilo ni la kihistoria kwa taifa lao, akibainisha kuwa huo ulikuwa ni mara ya kwanza kwake kukutana ana kwa ana na Rais Trump.

Hatua hiyo imekuja wiki chache baada ya vikosi vya Marekani kumkamata Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, mjini Caracas, na baadaye kumshtaki kwa tuhuma zinazohusiana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kupitia mitandao ya kijamii, Rais Trump alithibitisha kupokea tuzo hiyo na kutoa shukrani, akieleza kuwa kitendo hicho ni ishara ya heshima na uhusiano wa pande zote.

Hata hivyo, Trump ameendelea kusisitiza kutomuunga mkono Machado kama kiongozi mpya wa Venezuela, licha ya madai ya harakati zake kwamba alishinda uchaguzi wa 2024 uliokuwa na ushindani mkubwa.

FAHAMU TEKNOLOJIA MPYA ITKAYOTUMIKA KWENYE KAMBI – NGUVU za KIUME ZATAJWA TANLINK

Leave a Comment