×

CCM Yajipanga Kusimamia Serikali Kupitia Ziara ya Kitaifa – Video

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uwenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Labani Kihongosi

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuthibitisha kwa vitendo kuwa ndicho chama cha wananchi, baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uwenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Labani Kihongosi, katangaza kuanza kwa ziara ya kichama ya kitaifa itakayohusisha mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari Januari 17, 2026 katika Ukumbi wa Jakaya Convention Centre jijini Dodoma, Ndugu Kihongosi amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kuendelea kushirikiana na wananchi na wanachama wa CCM katika kulinda amani, umoja na maendeleo ya Taifa, sambamba na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi moja kwa moja.Alisema Ndugu Kihongosi;

“Kama chama, tuna wajibu wa kwenda kuisimamia Serikali. CCM ni chama cha watu, na hatuwezi kuongoza kwa kusikia taarifa za mezani pekee. Lazima tushuke kwa wananchi, tusikilize kero zao na kuzitatua.”

Amefafanua kuwa CCM ni chama cha kimaendeleo na chama cha kijamii, kinachojengwa juu ya misingi ya amani, umoja, mshikamano na kulinda utu wa Mtanzania, na kwamba misingi hiyo ndiyo iliyokiwezesha chama kukiongoza Taifa kwa muda mrefu kwa uthabiti na amani.Alisisitiza kwa kusema;

“CCM ni chama kinachopenda amani, kinacholinda utu wa Mtanzania na kinachotanguliza maslahi ya Taifa mbele ya maslahi binafsi au makundi. Hatujengi taifa kwa chuki wala migawanyiko.”

MNEC ameongeza kuwa CCM kimefurahishwa sana na hatua ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya kikao cha kufungua mwaka na Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali, akisema hatua hiyo imeongeza heshima ya Taifa letu kimataifa na kuwapa faraja wanachama wa CCM kote nchini.
Ameeleza kuwa kupitia ziara hiyo, chama kitashuka kwa wananchi kusikiliza na kutatua kero zote za wananchi, huku kikitathmini kwa kina utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Mheshimiwa Rais, na kuhakikisha maslahi ya wananchi yanalindwa na hayapotoshwi kwa namna yoyote.

Leave a Comment