The House of Social Media
gunners X

Waziri Wa Ulinzi Na Jeshi La Kujenga Taifa Atembelea Makao Makuu Ya Ulinzi Wa Taifa 

0
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Rhimo Simeon Nyansaho, Leo  tarehe 20 amefanya ziara katika  Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa ( MMUT), Kikombo  pamoja na Hospitali Kuu ya Rufaa ya Jeshi Msalato,  Jijini Dodoma.
Mhe. Nyansaho alianza kwa kutembelea MMUT  ambapo alipokelewa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman.
Akiwa MMUT, Waziri Nyansaho alitembelea ofisi mbalimbali zilizopo katika jengo hilo na kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi huo wa ujenzi ulioanza rasmi mwaka 2020.
Baada ya kumaliza ziara yake MMUT, Waziri Nyansaho alielekea katika Hospitali  Kuu ya Rufaa ya Kijeshi iliyoko Msalato ambapo pia alipata wasaa wa kuona ni kwa namna gani mradi huo umefikia katika hatua nzuri.
Mhe. Waziri Nyansaho, amefurahishwa na ujenzi wa Hospitali hiyo ya Jeshi na amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Hospitali yenye uwezo wa kutoa huduma nzuri na za kiwango cha juu   za matibabu  hasa katika  Jiji la Dodoma na hivyo kukamilika kwa Hospitali hiyo kutahakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya Jijini Dodoma
Waziri huyo amemaliza ziara yake  huku akilipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa hatua iliyofikiwa katika miradi hiyo miwili.
Leave A Reply