×

Victor Mhagama Aongoza Kura za Maoni CCM Jimbo la Peramiho

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songea Vijijini, jana Januari 21, 2026 kiliendesha zoezi la upigaji wa kura za maoni kwenye Kata 16 za Jimbo la Peramiho, ambapo Victor Mhagama aliibuka mshindi kwa kupata kura 3,040

Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa, jumla ya wapiga kura waliosajiliwa walikuwa 9,267, ambapo kura 9,167 zilipigwa. Kati ya hizo, 590 ziliharibika, hivyo kufanya idadi ya kura halali kufikia 8,577.

Aidha, Getrude Haule alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,913, akifuatiwa na Kizito Mhagama aliyepata kura 943.

Wengine ni Joseph Masikitiko (126), Erasmo Mwingira (124), Allen Mhagama (114), Schoral Ngonyani (84), Lazaro Ndenji (68), Davis Ngonyani (62), Thea Ntara (57), Emil Ngaponda (51), Serafina Mkuwa (48), Clemence Mwinuka (35), Emelian Mbawala (24), Benjamin Kamtawa (23), Prosper Luambano (22), Dominic Mahundi (19), Fredrick Millinga (17), Sixmund Rungu (9), Rose Shawa (7), Rosemary Ngonyani (6), na Enoc Moyo (6), ambao wote kwa pamoja walipata kura 1,681.

Imeelezwa baada ya matokeo hayo, vikao vya uamuzi ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa vitakaa kisha kuteua Mgombea atakayewakilisha Chama kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge.

Zoezi hili la kura za maoni lilifanyika kwa lengo la kumpata mrithi wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Peramiho, kufuatia kufariki kwa Mbunge aliyekuwa akiwakilisha Jimbo hilo, Marehemu Jenista Joakim Mhagama

Leave a Comment