The House of Social Media
gunners X

UNDP Tanzania Yawazawadia Wanafunzi Wajasiriamali

0
Ni 20 Zaidi ya Shilingi Milioni 70 Kupitia Awamu ya Pili ya Programu ya Youth Ignite Student Founders Fellowship
Dar es Salaam, Tanzania. Januari 30, 2026. Wanafunzi wajasiriamali ishirini kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wamepatiwa zawadi za fedha taslimu zaidi ya Shilingi milioni 70 kufuatia shindano la uwasilishaji wa mawazo ya biashara lililofanyika chini ya mpango wa Youth Ignite Student Founders Fellowship – Awamu ya Pili, unaotekelezwa kupitia Programu ya FUNGUO iliyo chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, kwa ufadhili wa pamoja wa Serikali ya Uingereza – kupitia Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO), Umoja wa Ulaya (EU) na serikali ya Finland.
Hafla hiyo ya uwasilishaji wa mawazo ya biashara iliwakutanisha pamoja wanafunzi 30 kutoka taasisi za elimu ya juu kutoka vyuo tofauti Tanzania, waliowasilisha mawazo bunifu ya biashara yenye mchango chanya kwa jamii mbele ya jopo la majaji. Tukio hili limekuwa hatua muhimu katika kuimarisha ujasiriamali na ubunifu miongoni mwa vijana nchini. Mbali na ushindi wa zawadi za fedha taslimu, wanafunzi wajasiriamali pia walipokea msaada wa kitaalamu, ikiwemo mafunzo ya maendeleo ya biashara, ushauri elekezi (mentorship), na maandalizi ya kuwafanya wawe tayari kuvutia wawekezaji wapya.
Mgeni Rasmi, Dkt. Harun Makandi, Mkurugenzi Msaidizi wa Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, alisisitiza jinsi mpango huo unavyoendana na ajenda ya Serikali ya kukuza ubunifu, utafiti wenye tija kibiashara, na ujasiriamali miongoni mwa vijana.
“Mpango huu unaunga mkono moja kwa moja jitihada za serikali za kulea kizazi kipya cha wabunifu na wazalishaji wa ajira mpya kinachotoka katika taasisi zetu za elimu ya juu. Unaakisi mwelekeo wa Tanzania wa kuunganisha sayansi, teknolojia na ujasiriamali katika maendeleo ya taifa,” alisema Dkt. Makandi.
Akitoa hotuba kuu, John Rutere, Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, alieleza jinsi ushirika huo unavyochangia malengo ya muda mrefu ya maendeleo ya Tanzania.
“Jukumu la UNDP nchini Tanzania limejikita katika kuunga mkono Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 (DIRA 2050), ambayo imeweka lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati cha juu kwa kufikia kiwango cha uchumi wenye thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni moja ifikapo mwaka 2050. Kufikia dira hii kunahitajika uwekezaji wa makusudi kwa vijana na biashara zao. Programu kama Youth Ignite Student Founders Fellowship ni mifano halisi ya miradi iayoongeza chachu inayowawezesha vijana kwa ujuzi, mitandao ya wawekezaji na mitaji wanayohitaji kujenga biashara zenye uwezo wa kukua na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.”
Washirika wa maendeleo walichangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kundi hili la washiriki. Bw. Euan Davidson, Kiongozi wa Timu ya Miradi Endelevu katika Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza (FCDO), alizungumza kwa niaba ya juhudi za maendeleo za Uingereza, akisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika biashara zinazoongozwa na vijana kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi jumuishi.
Westerwelle Foundation Tanzania na StartHub Africa zilichangia programu kwa kuwapatia washiriki
Leave A Reply