×

Rais Samia Akaribisha Rais wa Uganda Museveni Ikulu Dar (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 07 Februari, 2026.

Dar es Salaam, Tanzania – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo, tarehe 07 Februari 2026, mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu.

Ziara hii inafuata mahusiano ya kidiplomasia yanayokua kati ya Tanzania na Uganda, ambapo pande zote mbili zinatarajia kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, miundombinu, kilimo, na usalama wa kikanda.

Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar.

Rais Samia na Rais Museveni walipokelewana kwa heshima kubwa, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kupokea wageni rasmi wa mataifa jirani, kabla ya kuanza mazungumzo ya kidiplomasia ya pamoja. Mazungumzo haya yanatarajiwa kujadili masuala ya kibiashara, uhusiano wa kikanda, na juhudi za pamoja za maendeleo.

Ziara ya Rais Museveni ni ishara ya dhahiri ya ushirikiano thabiti kati ya Tanzania na Uganda, na inatarajiwa kuchangia katika kuimarisha amani, utulivu, na maendeleo ya kikanda kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili.

Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni.Yoweri Kaguta Museveni.

Leave a Comment