×

Halmashauri ya Mwanga Yatangaza Nafasi 9 za Ajira kwa Watanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ametangaza waziwazi fursa za ajira tisa (9) kwa Watanzania wenye sifa, baada ya kupata kibali cha Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Nafasi hizo ni pamoja na:

  • Dereva Daraja la II – Nafasi 5

  • Mwandishi Mwenda Ofisi II – Nafasi 4

Sifa Muhimu za Waombaji

  • Kuwa raia wa Tanzania na umri si zaidi ya miaka 45.

  • Kwa Madereva: Form IV + leseni ya Daraja E au C na uzoefu wa angalau mwaka 1 bila ajali.

  • Kwa Waandishi Mwenda Ofisi: Form IV au VI + Diploma/Uhazili au NTA Level 6 + ujuzi wa kompyuta na lugha.

  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba.

 Masharti ya Jumla

  • Waombaji wote watalazimika kuambatisha C.V, vyeti vya elimu vilivyothibitishwa, na vyeti vya mafunzo husika.

  • Vyeti vya masomo ya nje ya Tanzania lazima viidhinishwe na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTE).

  • Waombaji waliostaafuwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

  • Mwisho wa kuwasilisha maombi: 20 Februari 2026.

 Jinsi ya Kuomba

Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielectroniki wa Ajira kwa https://portal.ajira.go.tz. Maombi yasiyo tumwa kwa njia hii hayatazingatiwa.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, S.L.P 716, Mwanga
Simu: +255 26 2757652 | Nukushi: +255 26 2756463

Leave a Comment