
Kwa niaba ya Wakala wa Huduma za Ufundi za Umeme, Mitambo na Elektroniki Tanzania (TEMESA), Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa, weledi, uadilifu na ari ya kufanya kazi kujaza nafasi sita (6) za kazi kama ifuatavyo:
1. Nafasi: Meneja wa Kanda (Regional Manager) – Nafasi 6
Majukumu ya Kazi
-
Kusimamia uendeshaji wa shughuli za kanda kwa ufanisi na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati na kwa viwango vya ubora.
-
Kusimamia rasilimali za kazi zikiwemo vifaa, zana na mitambo bila kuzalisha gharama zisizo za lazima.
-
Kuboresha huduma kwa wateja kwa kuhakikisha malalamiko yanashughulikiwa haraka.
-
Kuongoza na kusimamia wasimamizi pamoja na wafanyakazi wa utawala.
-
Kuandaa na kusimamia bajeti ya kanda kwa kuzingatia matumizi yenye tija.
-
Kuratibu mafunzo kwa watumishi wa kiufundi ili kuongeza ujuzi.
-
Kushirikiana na timu za kiufundi kuboresha utoaji huduma.
-
Kutafuta fursa za kibiashara na kupanua wigo wa huduma za TEMESA ndani ya kanda husika.
-
Kujenga mahusiano mazuri na wadau, jamii na mamlaka za eneo.
-
Kuandaa taarifa za utendaji wa kanda mara kwa mara.
-
Kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na msimamizi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji anatakiwa kuwa na:
-
Shahada ya Uzamili na Shahada ya Kwanza katika mojawapo ya fani zifuatazo:
Biashara (Fedha/Marketing), Fedha, Uchumi, Takwimu, Utawala wa Umma, au Uhandisi (Umeme, Mitambo, Elektroniki, Electromechanical). -
Waombaji wa Uhandisi lazima wawe wamesajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kama Professional Engineer.
-
Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 8 katika fani husika.
-
Shahada ya Uzamili inayohusiana na Shahada ya Kwanza ni faida zaidi.
Mshahara
TMSS 10
Masharti ya Jumla
-
Mwombaji awe raia wa Tanzania na asiwe na umri zaidi ya miaka 45.
-
Aambatanishe nakala zilizothibitishwa za vyeti vyote muhimu (elimu, taaluma, cheti cha kuzaliwa n.k).
-
Wasitumie result slips, testimonials au partial transcripts.
-
Aweke picha ya passport size ya hivi karibuni.
-
Waajiriwa wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba.
-
Aonyeshe majina ya wadhamini (referees) watatu.
-
Vyeti vya nje ya nchi vihalalishwe na TCU/NECTA/NACTVET.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote yawasilishwe kupitia Recruitment Portal ya PSRS pekee.
Mwisho wa Kutuma Maombi: 20 Februari, 2026
Katibu,
Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
S.L.P 2320, Dodoma.