
USIKU wa kuamkia leo Februari 13, 2026, burudani ilihamia rasmi katika ukumbi wa Mlimani City Conference Centre, ambapo hafla kubwa ya Tanzania Creator’s Awards ilifanyika kwa shamrashamra, vicheko na shangwe zisizo na kifani.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na mastaa, wabunifu wa maudhui ya mtandaoni, wanahabari pamoja na viongozi mbalimbali wa sekta ya sanaa na filamu.

Mgeni rasmi alikuwa Dkt. Gervas Kasiga, Katibu Mtendaji wa Tanzania Film Board, aliyesisitiza umuhimu wa wabunifu wa kidijitali katika kukuza uchumi wa ubunifu nchini.
Uzito wa hafla uliongezeka zaidi kwa uwepo wa Mbunge wa Buchosa na Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo, pamoja na wadau wengine wakubwa wa tasnia.
Washindi waliotikisa ukumbi
-
Best Online Media 2025 – Global TV Online walitwaa tuzo hiyo, jambo lililosababisha shangwe kubwa ukumbini.
-
Best Comedian – Anko Nzala aliibuka kidedea, akishangiliwa kwa nguvu na mashabiki.
-
People’s Choice MC of the Year – Mc Gara B alishukuru mashabiki kwa sapoti kubwa aliyopata.

Miongoni mwa waliopendezesha usiku huo walikuwa:
-
Fatma Dewji, dada wa mwekezaji wa Simba Sports Club
-
Mwigizaji na staa wa burudani Kajala Masanja
-
pamoja na wasanii na ma-creator wengine
Kwa kifupi, ilikuwa ni usiku wa heshima, vipaji na ushindi, ukionyesha jinsi tasnia ya uundaji maudhui mtandaoni Tanzania inavyokua kwa kasi. Tuzo hizi zimekuwa jukwaa muhimu la kutambua juhudi za wabunifu na kuwapa motisha waendelee kung’ara.







HABARI / PICHA NA RICHARD BUKOS GPL