
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imetangaza nafasi nane (08) za ajira baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Soma zaidi hapa>>>NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA
Nafasi Zilizotangazwa
1️⃣ Dereva Daraja la II – Nafasi 06
Majukumu:
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari
-
Kuwapeleka watumishi safari za kikazi
-
Kufanya matengenezo madogo ya gari
-
Kusambaza nyaraka
-
Kujaza daftari la safari
-
Kufanya usafi wa gari
-
Kazi nyingine atakazopangiwa
Sifa:
-
Elimu ya Kidato cha Nne
-
Leseni Daraja C au E
-
Uzoefu wa angalau mwaka mmoja bila kusababisha ajali
-
Cheti cha Basic Driving Course kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa
Mshahara: TGS B
2️⃣ Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 02
Majukumu:
-
Kuchapa barua na nyaraka (za kawaida na siri)
-
Kupokea na kuwaelekeza wageni
-
Kutunza kumbukumbu za ofisi
-
Kupanga majalada na maandalizi ya vikao
-
Kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi
-
Kazi nyingine atakazopangiwa
Sifa:
-
Kidato cha Nne
-
Stashahada (NTA Level 6) ya Uhazili
-
Ujuzi wa Shorthand (80 w.p.m) Kiswahili na Kiingereza
-
Ujuzi wa kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher)
Mshahara: TGS C
📌 Masharti ya Jumla
-
Mwombaji awe raia wa Tanzania (miaka 18–45)
-
CV kamili na wadhamini watatu
-
Vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
-
Waombaji waliostaafu au watumishi wa umma wafuate taratibu maalum
-
Vyeti vya nje ya nchi vithibitishwe na TCU/NACTE/NECTA
-
Maombi ya kughushi hayatavumiliwa
🗓 Mwisho wa kupokea maombi: 05 Machi, 2026
📩 Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa Ajira (Recruitment Portal):
👉 https://portal.ajira.go.tz/
Barua ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela
S.L.P 320, Kyela – Mbeya