×

Simulizi ya Kusikitisha ya Punch the Monkey, Akataliwa na Mama Yake, Ateka Mitandao – Video

Punch the Monkey amekuwa gumzo mtandaoni baada ya video zake kuenea kwa kasi, zikimuonesha akiwa ameshikilia mdoli wake wa kitambaa kwa upendo mkubwa jambo lililogusa mioyo ya watu wengi. Lakini nyuma ya umaarufu huo, kuna simulizi ya kusikitisha inayofichua mapambano yake tangu utotoni.

Punch, ambaye ni tumbili aina ya capuchin, alikataliwa na mama yake muda mfupi baada ya kuzaliwa. Kwa wanyama wa jamii ya primates, uhusiano kati ya mama na mtoto huwa wa karibu sana, hasa katika miezi ya mwanzo ya maisha. Kukosa mapenzi na ulinzi wa mama katika hatua hiyo kunaweza kuathiri sana ukuaji wa kihisia na kitabia wa mtoto.

Wataalamu wa wanyama wanasema hali kama hiyo inaweza kusababishwa na msongo wa mawazo kwa mama, kutokuwa na uzoefu, au changamoto za kiafya. Kwa Punch, kukataliwa kulimaanisha kuishi maisha ya kulelewa na binadamu ili kuokoa uhai wake.

Moja ya vitu vilivyowagusa wengi ni jinsi Punch alivyoambatana na mdoli wake ambao umekuwa kama mbadala wa upendo wa mama alioukosa. Kitaalamu, wanyama waliotenganishwa na wazazi wao mapema huweza kuonyesha tabia ya kushikamana na vitu vinavyowapa faraja.

Kadri Punch alivyokua, changamoto ziliongezeka. Alipokuwa akijaribu kujiunga na kundi la tumbili wenzake, alikumbana na ugumu mkubwa. Tumbili wa capuchin huishi katika makundi yenye mpangilio maalum wa uongozi na kanuni kali za kijamii.

Kwa kuwa Punch alikuzwa na binadamu, alikosa kujifunza baadhi ya ishara na tabia za kawaida za kijamii za jamii yake. Hali hii ilimfanya ashindwe kuendana na wenzake, na mara kadhaa aliripotiwa kushambuliwa au kutengwa.

Bustani ya wanyama ya Ichikawa City Zoological and Botanical Gardens imetoa tamko rasmi kuhusu video zilizosambaa mitandaoni zikimuonesha tumbili mtoto maarufu, Punch, akionekana kama anashambuliwa na tumbili wengine.

Lakini uongozi wa bustani hiyo umeomba mashabiki wasimwonee huruma kupita kiasi.

Katika taarifa yao, wamesema:

  • Punch anaingizwa rasmi ndani ya kundi (troop) la tumbili wa Kijapani (Japanese macaques).

  • Wataratibu walitarajia changamoto kama hizo wakati wa kumzoesha kuishi na kundi.

  • Ingawa amekaripiwa mara kadhaa na tumbili wakubwa, hakuna aliyeonesha ukatili wa kumuumiza kwa kiwango kikubwa.

  • Tabia zinazoonekana kwenye video ni sehemu ya kawaida ya mfumo wa kijamii wa tumbili.

Kwa tumbili wa Kijapani, watoto hujifunza kupitia:

  • Kuheshimu mpangilio wa madaraka (hierarchy)

  • Kanuni za mawasiliano

  • Namna ya kuishi na kushirikiana na wengine

Bustani imesisitiza kuwa Punch anaonesha ustahimilivu na nguvu ya kisaikolojia, na badala ya kumwonea huruma, mashabiki wanapaswa kumuunga mkono katika hatua yake ya kujifunza kuishi ndani ya kundi.

Hata hivyo, watumiaji wa mitandao bado wanaonesha hisia kali wanapomuona tumbili mdogo akikaripiwa au kusukumwa. Ni jambo linalogusa hisia kwa wengi.

Lakini kwa mujibu wa wataalamu wa bustani hiyo, Punch yuko salama na anapitia mchakato wa kawaida wa ukuaji na jinsi ya kujifunza katika jamii ya tumbili.

Leave a Comment