×

Magari Yaponea Chupu Chupu Kuzama Shimoni Baada ya Barabara Kupasuka – Video

Magari mawili  yameponea chupuchupu  kuzama kwenye shimo kubwa lililopasuka mfuniko ghafla kwenye makutano ya barabara katika Jimbo la Nebraska, Marekani, Februari 24, 2026.

Kwa mujibu wa video ya kamera ya polisi trafiki, magari hayo yalikuwa yamesimama kwa utulivu yakisubiri taa za kuongozea magari zibadilike. Hata hivyo, bila dalili yoyote ya hatari, sehemu ya barabara ilianza kuporomoka ghafla na kutengeneza shimo kubwa lililofanya sehemu ya magari hayo kutumbukia shimoni.

Tukio hilo lilitokea kwa sekunde chache na kusababisha taharuki kwa madereva na wapita njia waliokuwepo eneo hilo. Baada ya muda mfupi, watu waliokuwa karibu pamoja na madereva wengine walikimbilia kutoa msaada kwa waliokuwa ndani ya magari hayo.

Kwa bahati nzuri, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya ndani, hakuna mtu aliyeripotiwa kujeruhiwa katika tukio hilo.

Polisi wamefunga barabara hiyo kwa siku kadhaa ili kuruhusu uchunguzi na matengenezo kufanyika, wakionya kuwa shimo hilo linaweza kuendelea kupanuka na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.

Leave a Comment