
Katika ulimwengu wa teknolojia, watu wengi wamezoea kutumia Google Chrome au Mozilla Firefox kama chaguo la kwanza la kuvinjari mtandao. Hata hivyo, kuna browser mbadala ambazo zimekuwa zikivutia watumiaji kutokana na wepesi wake, faragha (privacy), na ubunifu wake. Hizi hapa ni baadhi ya browser za “kijanja” zinazotajwa mara nyingi:
1. Inkbrow (Inkbrowser)
Inkbrowser ni browser nyepesi inayolenga zaidi faragha ya mtumiaji.
Sifa Kuu:
-
Haina matangazo mengi yanayokusumbua.
-
Ina mfumo wa “incognito” ulioimarishwa.
-
Ni nyepesi, hivyo haichukui RAM kubwa kwenye simu.
-
Inafaa kwa simu zenye uwezo mdogo.
Kwa wanaopenda usiri na kasi bila vitu vingi vya ziada, Inkbrowser ni chaguo zuri.
2. Soul Browser
Soul Browser imepata umaarufu mkubwa hasa kwa watumiaji wa Android.
Sifa Kuu:
-
Ina uwezo wa kupakua video moja kwa moja kutoka baadhi ya tovuti.
-
Ina ad blocker iliyojengewa ndani.
-
Inaruhusu kubadilisha muonekano (customization) kwa mapenzi yako.
-
Ina night mode na font size adjustment kwa urahisi.
Kwa wanaopenda udhibiti mkubwa wa browser yao na vipengele vya ziada, Soul ni moja ya bora.
3. Pawxy Browser
Pawxy Browser ni browser nyingine inayolenga faragha na matumizi madogo ya data.
Sifa Kuu:
-
Ni nyepesi na rahisi kutumia.
-
Ina uwezo wa kuzuia matangazo (ad blocking).
-
Inasaidia kuokoa data.
-
Inafaa kwa watumiaji wanaotaka browser isiyo na mambo mengi magumu.
4. Microsoft Edge
Browser bora kama unahitaji zana za faragha zilizo wazi
Kwa nini ni nzuri:
-
Ina mipangilio ya faragha iliyojengwa ndani inayokuwezesha kuchagua kiwango cha ulinzi unachotaka.
-
Ina kinga dhidi ya ufuatiliaji (tracking prevention) ambayo huzuia tovuti kukusanya taarifa zako bila ruhusa.
-
Ina dashibodi ya faragha iliyo wazi, hivyo unaweza kuona na kubadilisha mipangilio kwa urahisi.
-
Inafanya kazi vizuri kwenye Windows, na pia inapatikana kwa macOS, iOS na Android.