×

Senegal Wanyang’anywa Ubingwa wa AFCON, Morocco Washinda Mezani

Shirikisho la Soka Barani Afrika,(CAF), kupitia Kamati yake ya Rufaa, limetangaza rasmi kuwa timu ya taifa ya Senegal National Football Team imepoteza mechi ya fainali ya AFCON 2025 kwa njia ya forfeit, na hivyo ushindi wa mabao 3–0 kutolewa kwa Morocco National Football Team.

Uamuzi huo umetokana na rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la mpira wa miguu la Morocco(FRMF), ambapo Kamati ya Rufaa ilibatilisha uamuzi wa awali wa Kamati ya Nidhamu ya CAF na kuunga mkono rufaa hiyo.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, Senegal ilikiuka Kanuni za AFCON, hususan Kifungu cha 82 na 84, jambo lililosababisha timu hiyo kuadhibiwa kwa kupoteza mechi hiyo rasmi. Aidha, Fédération Sénégalaise de Football (FSF) ilibainika kuwajibika kwa mwenendo wa timu yao uliokiuka kanuni hizo.

Leave a Comment