Moshi ilichangamka kwa maelfu ya wakimbiaji na mashabiki walioshiriki Kilimanjaro Marathon 2026, tukio linaloendelea kuunganisha michezo, utalii na jamii nchini Tanzania.
Mbio hizo zimezidi kukua kimataifa, zikivutia washiriki wa ndani na nje ya nchi, huku zikitoa mchango mkubwa kwa uchumi wa Moshi kupitia sekta za hoteli, usafiri na biashara ndogo.Mafanikio hayo yanaungwa mkono na Tanzania Breweries PLC kupitia chapa yake ya Kilimanjaro Lager, ambayo imeendelea kudhamini tukio hilo kwa miaka mingi.
Mbali na uchumi, marathon hii imeendelea kuhamasisha afya, kuimarisha mshikamano wa jamii, na kuitangaza Tanzania kimataifa kama kitovu cha utalii wa michezo.

Akizungumza baada ya tukio, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Michelle Kilpin, alisema marathon hiyo inaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwaleta watu pamoja, kukuza utalii na kuhamasisha maisha yenye afya.
