×

Serikali Yatangaza Nafasi 158 za Kazi Katika Taasisi Mbali Mbali za Umma

Taasisi mbalimbali za umma nchini zimetangaza nafasi za ajira 158 katika kada tofauti  Shirika la Posta Tanzania (TPC), Ofisi ya Viwango Tanzania (TBS), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Watumishi Housing Investments (WHI), Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA), Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Njombe (NJUWASA),

Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE), Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Taasisi ya Mafunzo ya Serikali za Mitaa (LGTI),

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 04 Aprili, 2026. Kusoma nafasi zote zilizotangazwa bonyeza link hapa chini

 

 NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 22-03-2026

🔹 1. TANZANIA POSTS CORPORATION (TPC)

✅ Driver II – Nafasi 20

Majukumu:

  • Kuendesha magari ya shirika
  • Kutunza logbook za safari
  • Kuhakikisha usalama na usafi wa gari
  • Kuripoti hitilafu za gari mapema
  • Kufanya matengenezo madogo

Sifa:

  • Elimu ya Kidato cha Nne
  • Leseni daraja C au E
  • Mafunzo ya udereva (VETA)
  • Uzoefu angalau mwaka 1 bila ajali

Mshahara: TPCSS 2

✅ Clearing and Forwarding Officer II – Nafasi 1

Majukumu:

  • Kushughulikia nyaraka za usafirishaji
  • Kutambua nyaraka pungufu
  • Kupendekeza HS Code
  • Kuandaa taarifa za forodha kwa Tanzania Revenue Authority

Sifa:

  • Shahada ya Clearing and Forwarding

Mshahara: TPCSS 4

🔹 2. TANZANIA BUREAU OF STANDARDS (TBS)

✅ Laboratory Assistant II – Nafasi 17

Majukumu:

  • Kuandaa reagents rahisi
  • Kusafisha vifaa vya maabara
  • Kuandaa sampuli
  • Kuhakikisha usalama wa maabara

Sifa:

  • Kidato cha Nne + Cheti cha maabara (NVA Level II/III au Trade Test)

Mshahara: TBSS 2

✅ Quality Assurance Officer II (Chemistry) – Nafasi 2

Majukumu:

  • Kufanya uchambuzi wa sampuli
  • Kusimamia ubora wa bidhaa
  • Kufanya tafiti na mafunzo
  • Kutekeleza mifumo ya ubora

Sifa:

  • Shahada ya Kemia

Mshahara: TBSS 4

🔹 3. UNIVERSITY OF DODOMA (UDOM)

✅ Driver II – Nafasi 3

Majukumu:

  • Kuendesha magari ya chuo
  • Kufanya ukaguzi wa gari kabla ya safari
  • Kutunza kumbukumbu za safari
  • Kuripoti ajali au hitilafu

Sifa:

  • Kidato cha Nne/Sita
  • Leseni C au E
  • Mafunzo ya udereva (VETA)
  • Uzoefu wa mwaka 1

Mshahara: PGSS 2.1

✅ Admission Officer II (Statistics) – Nafasi 3

Majukumu:

  • Kusimamia udahili wa wanafunzi
  • Kuchambua takwimu za waombaji
  • Kusimamia usajili wa wanafunzi
  • Kuhifadhi taarifa za wanafunzi….

Endelea kusoma nafasi zilizotangazwa bonyeza link hapa chini:-

 NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 22-03-2026

Leave a Comment