×

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile Atenguliwa – Video

Dkt. James Andilile Mwainyekule aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Aprili 2, 2026 amefanya mabadiliko katika uongozi wa EWURA kwa kumwondoa Dkt. James Andilile Mwainyekule katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Dkt. Mwainyekule ameondolewa katika wadhifa huo na anatarajiwa kupangiwa majukumu mengine ndani ya utumishi wa umma.

Hadi sasa, haijaelezwa rasmi nani atachukua nafasi hiyo, huku wadau wakisubiri uteuzi mpya utakaoongoza mamlaka hiyo nyeti inayosimamia huduma za nishati na maji nchini.

Leave a Comment