
MSANII wa Bongo Muvi, Agness Suleiman Kihamba maarufu kama Aggy Baby, amesema kuwa kwa sasa mahari yake imefikia Shilingi bilioni 1.5, akieleza kuwa thamani yake imeongezeka kutokana na kukua kiakili na uzoefu wa maisha.
Akizungumza katika mahojiano na Dadaz, Aggy Baby alisema tofauti na mwaka jana ambapo mahari yake ilikuwa bilioni 1, kwa sasa ameongeza kiwango hicho kwa sababu anaamini ana thamani kubwa zaidi kwa mwanaume atakayemuoa.

“Ninavyozidi kukua ndivyo ninavyozidi kupanuka kiakili, na hiyo ni tunu muhimu kwa mwanaume atakayenioa,” alisema.
Aidha, amesisitiza kuwa mahari hiyo inalipwa kwa mkupuo (full payment), bila malipo ya awamu.
Mbali na hilo, Aggy Baby amedai kuwa kuna mchezaji wa Manchester United anayemsumbua kimapenzi kupitia ujumbe binafsi (DM), akisema tayari amempa onyo la mwisho.
Ameongeza kuwa endapo mchezaji huyo hataacha, yuko tayari kumtaja hadharani na kuweka wazi ujumbe wake, akibainisha kuwa ni mchezaji kutoka Ulaya anayekipiga katika klabu hiyo.
Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa mitandaoni huku wengi wakisubiri kuona kama atafichua jina la mchezaji huyo.
