
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, ametoa kauli hiyo Aprili 2, 2026, wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Hotuba hiyo iliwasilishwa bungeni na Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, ambapo wabunge mbalimbali walipewa nafasi ya kuchangia na kutoa maoni yao kuhusu vipaumbele vya serikali.
Katika mchango wake, Shigongo aligusia masuala muhimu yanayohusu maendeleo na ustawi wa wananchi, akisisitiza umuhimu wa serikali kuendelea kuboresha huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.