
Simba leo Aprili 9, 2026 ameshindwa kupata ushindi kwa mara ya kwanza dhidi ya TRA United baada ya kulazimishwa sare tasa (0-0) katika dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha. Ni matokeo ambayo yanaongeza presha kwenye mbio za ubingwa kwa upande wao.
Simba sasa wanaendelea kushikilia nafasi ya pili wakiwa alama 8 nyuma ya vinara Yanga (wana alama 4️⃣4️⃣)
, ambao wana alama 3️⃣6️⃣ baada ya kucheza mechi 17 (na mechi moja pungufu). Hii inaifanya mbio za ubingwa kuwa ngumu zaidi kwa Simba, ambapo kila mchezo unaobaki unakuwa muhimu sana.

Kwingineko, Azam FC nao walilazimishwa sare tasa dhidi ya Mbeya City FC katika dimba la Tanzanite Kwaraa, Babati Manyara. Matokeo hayo yanawaacha wote wakigawana pointi moja kila mmoja.
📊 FT Results:
- TRA United 0-0 Simba SC 🟥 (Nouma 87’)
- Mbeya City 0-0 Azam FC
MSIMAMO – NBC PL 🇹🇿
1. Yanga – Pts 4️⃣4️⃣ (Mechi 18)
2. Simba – Pts 3️⃣6️⃣ (Mechi 17)
3. Azam – Pts 3️⃣4️⃣ (Mechi 18)
4. JKT – Pts 2️⃣9️⃣ (Mechi 18)