×

Dkt. Mwigulu Nchemba Aongoza Harambee ya Mei Mosi 2026 – Yachangwa Bilioni 1.105

Waziri Mkuu wa Mwigulu Nchemba ameongoza rasmi harambee ya kuchangia maandalizi ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2026, ambazo mwaka huu kitaifa zitafanyika mkoani Njombe.

Harambee hiyo iliyofanyika Aprili 13, 2026 imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 1.105, fedha ambazo zitaelekezwa katika maandalizi ya sherehe hizo muhimu kwa wafanyakazi nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mkuu amepongeza ushirikiano wa wadau mbalimbali waliotoa michango yao kwa ajili ya kufanikisha maadhimisho hayo, akisisitiza umuhimu wa kuenzi mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya taifa.

Maadhimisho ya Mei Mosi huadhimishwa kila mwaka duniani kote, yakilenga kutambua mchango wa wafanyakazi katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.

Leave a Comment