×

SBL Yazindua Serengeti Apple, Kinywaji cha Kwanza Chenye Ladha na Hadhi ya Kipekee Kilichotengenezwa Tanzania

Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua kinywaji kipya cha Serengeti Premium Apple, kikitajwa kuwa bidhaa ya kwanza ya aina ya Ready-to-Drink (RTD) kutengenezwa nchini Tanzania. Kinywaji hicho kimetengenezwa kwa ladha ya tufaa na kinalenga watumiaji wanaotafuta ubora, hadhi na ladha ya kisasa.

Uzinduzi wa bidhaa hiyo unatarajiwa kufanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ikiwa ni sehemu ya kuonesha fahari ya rasilimali za Tanzania na kuhusisha utalii katika kampeni ya chapa hiyo mpya.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Obinna Anyalebechi, amesema Serengeti Premium Apple imebuniwa kukidhi mahitaji ya watumiaji wanaotafuta ladha mpya, nyepesi na yenye kuburudisha, huku ikiwakilisha hadhi na usasa wa Mtanzania wa leo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ubunifu na Masoko wa SBL, Henry Esiaba, amesema uzinduzi huo utawakutanisha wabunifu wa maudhui, wanawake wenye ushawishi na wadau mbalimbali ili kuitangaza Tanzania pamoja na chapa hiyo mpya.

Leave a Comment