×

SuperSport Kurusha Mechi Zote 104 za Kombe la Dunia 2026 Mubashara Afrika

Shuhudia Historia ya Afrika Ikifanyika Duniani Huku SuperSport Ikirusha Mechi Zote 104 za Kombe la Dunia la FIFA 2026™️ Mubashara

SuperSport na DStv (kampuni tanzu za MultiChoice Group, kampuni ya CANAL+) zimejipanga kikamilifu kuwaletea wateja wao barani Afrika Kombe la Dunia la FIFA 2026™️ la kihistoria, kwa kurusha mechi zote 104 mubashara kutoka Mexico, Canada na Marekani. Mechi hizo zitapatikana kwa wateja wa DStv na DStv Stream.

17 Aprili 2026 – SuperSport, kampuni tanzu ya MultiChoice Group, kampuni ya CANAL+, kwa fahari kubwa inatangaza kuwa mtangazaji mkubwa zaidi wa michezo barani Afrika ataleta Kombe la Dunia la FIFA 2026™️ kubwa zaidi kuwahi kutokea, mubashara kwa watazamaji katika nchi zinazozungumza Kiingereza na Kireno barani Afrika.

Kwa mara ya kwanza katika historia, mashindano haya yatapatikana kwa ukamilifu kwa wateja wote wa DStv kuanzia kifurushi cha DStv Access hadi DStv Premium, yakijumuisha mechi zote 104 mubashara, matangazo ya muhtasari na marudio. Hili linaifanya FIFA World Cup 2026™️ kuwa Kombe la Dunia linalofikika zaidi kuwahi kutokea kwa wateja wa MultiChoice Group.

Mashindano haya, ambayo yamepanuliwa kushirikisha mataifa 48 kutoka 32, yataanza mjini Mexico City tarehe 11 Juni 2026 na kumalizika kwa fainali huko New Jersey tarehe 19 Julai 2026. Upanuzi huu unalifanya Kombe la Dunia la FIFA 2026™️ kuwa ndilo lililodumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya mashindano haya, likiwa na idadi kubwa zaidi ya mechi kuwahi kufanyika. Watazamaji wako tayari kushuhudia Kombe la Dunia lenye msisimko mkubwa kuliko yote.

Ili kuonesha ukubwa wa tukio hili kwa watazamaji na wateja wao barani Afrika, DStv ilishirikiana na nyota wa Hollywood Idris Elba – Kijana kutoka Ghana na Sierra Leone – ambaye alitangaza Jumatano kuwa mechi zote 104 zitakuwa zikirushwa mubashara kupitia DStv.

Historia ya Afrika
Afrika itapeleka msafara wake mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika bara la Amerika, huku mataifa 10 yakifuzu kupitia mashindano ya kufuzu ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Mataifa hayo 10 ya Afrika, ambayo bila shaka yataleta rangi, ladha na midundo ya kipekee ya ngoma za Afrika katika tamasha la kimataifa litakalofanyika Amerika Kaskazini, ni: Ghana, Afrika Kusini, Senegal, Cape Verde, Côte d’Ivoire, Misri, Algeria, Morocco, Tunisia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kuheshimu historia hii, SuperSport italeta vipindi vipya vya majarida ya michezo vyenye nyuso mpya, pamoja na vipindi maalum vya uchambuzi vitakavyoongozwa na wataalamu wa soka kutoka Afrika na duniani kote.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Rendani Ramovha, Mkurugenzi wa CANAL+ anayehusika na Maudhui na Michezo katika nchi zinazozungumza Kiingereza na Kireno barani Afrika, alisema:
“Tunayo furaha kubwa kutangaza kuwa wateja wetu katika Afrika inayozungumza Kiingereza na Kireno watapata fursa ya kushuhudia Kombe la Dunia lingine la kihistoria la FIFA kupitia Nyumbani kwa Mabingwa, SuperSport.

“Kwa Afrika kupeleka msafara wake mkubwa zaidi kwenda Mexico, Canada na Marekani, tunajivunia kuwaletea Waafrika jukwaa kubwa zaidi la michezo duniani kwa ubora wa SuperSport ambao wameuzoea. Kwa kuwa hili ndilo Kombe la Dunia lililosubiriwa kwa hamu kubwa zaidi kutoka mtazamo wa Afrika tangu mwaka 2010, tunafurahia kwamba watu wengi zaidi wataweza kutazama michuano hii kupitia kifurushi cha DStv Access.

“Pia tunatazamia kuwaletea wateja wetu vipengele maalum vya matangazo, vilivyolengwa kwa tamaduni za kipekee pamoja na baadhi ya lugha za Kiafrika.”
DStv iko tayari kuwapa wateja wake uzoefu wa kipekee wa utazamaji na huduma kwa wateja. Kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kutazama mechi zote 104 za Kombe la Dunia la FIFA 2026™️ mubashara, tembelea www.dstv.com au tumia programu ya MyDStv.

Kwa taarifa zote za Kombe la Dunia la FIFA™️ kupitia SuperSport, tembelea www.supersport.com.

(Nchi ambazo Kombe la Dunia la FIFA litapatikana kupitia SuperSport, kwa mpangilio wa alfabeti):

Angola
Botswana
Cape Verde
Equatorial Guinea
Eritrea
Eswatini
Ethiopia
Gambia
Ghana
Guinea Bissau
Kenya
Lesotho
Liberia
Malawi
Mauritius
Mozambique
Namibia
Nigeria
Rwanda
Sao Tome & Principe
Sierra Leone
South Africa
Tanzania
Uganda
Zambia

Leave a Comment