
MBUNGE wa Buchosa na mfanyabiashara, Eric Shigongo amesema kuwa wazo la kuanzisha Wezesha Mzawa Microfinance Ltd lilitokana na dhamira yake ya kusaidia Watanzania kupata mitaji ya haraka kwa ajili ya biashara.
Anabainisha kuwa takribani miaka kumi iliyopita alianza kufikiria suluhisho la changamoto ya ukosefu wa mitaji, ndipo akaanzisha kampuni hiyo kwa lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Kwa sasa, anasema kampuni imekua na inahudumia watu wengi wenye hali ngumu za maisha, ikiwasaidia kujikwamua kupitia mikopo.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya kampuni hiyo na Umoja wa Waendesha Bodaboda na Bajaj jijini Dar es Salaam.
Kupitia ushirikiano huo, madereva wa bodaboda na Bajaj watanufaika na mikopo yenye riba nafuu, hatua inayolenga kuboresha hali zao za kiuchumi na kukuza shughuli zao za usafirishaji.

Akizungumza katika kikao hicho, Shigongo amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji, akieleza kuwa uwepo wa mikopo na fursa za kifedha unaweza kusaidia kuboresha maisha ya wananchi wengi.
Shigongo ameshiriki kusaini kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya kampuni ya Wezesha Mzawa Microfinance na Uongozi wa Maafisa Usafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam, yenye lengo la kuwawezesha madereva bodaboda na Bajaj kiuchumi.
Kupitia makubaliano hayo, Wezesha Mzawa Microfinance imeanza rasmi kutoa mikopo kwa madereva hao, ikiwa ni pamoja na mikopo ya fedha taslimu pamoja na mikopo ya kuwawezesha kumiliki vyombo vyao vya usafirishaji.

Kwa upande wao, uongozi wa maafisa usafirishaji wa Dar es Salaam wameishukuru kampuni ya Wezesha Mzawa kwa kutoa mikopo kwa wakati kwa madereva wa bodaboda na bajaji, jambo ambalo wamesema limechangia kwa kiasi kikubwa kuinua kipato na kuboresha huduma za usafiri jijini.
Wezesha Mzawa Microfinance sehemu sahihi ya kupata mkopo kwa urahisi, haraka na kwa vigezo nafuu.
Tunatoa mikopo kuanzia Tsh 500,000 hadi Tsh 100,000,000 kulingana na mahitaji yako.


