×

Exim Bank Yaunga Mkono Juhudi Za Wizara Ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda.

Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutekeleza mageuzi makubwa ya elimu nchini, timu ya Benki ya Exim ikiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha Shani Kinswaga pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wa kati Andrew Lyimo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Stanley Kafu ilikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda.

Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, Aprili 27, 2026 kilikuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Benki ya Exim katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya elimu, zikiwemo fursa za ufadhili wa wanafunzi wa elimu ya juu hususan wanaosomea sayansi ya data (Data Science), akili unde (Artificial Intelligence) na sayansi shirikishi.

Majadiliano hayo pia yaliangazia fursa mbalimbali ikiwemo fursa za ufadhili unaoweza kutolewa na Benki hiyo, hususani kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaochukua masomo ya sayansi ya elimu ya data na akili.

Leave a Comment