×

Aliyemuua Mpenzi Wake Kwa Kumkataka Vipande Ahukumiwa Kunyongwa – Video

Abdalah Mussa maarufu Mr. bluu

MAHAKAMA Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa ‘Death by hanging’ Abdalah Mussa maarufu Mr. bluu, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Ezenia Kamana kwa kumkatakata vipande na kuvigawa katika mifuko nane ya salfeti na kuvitupa eneo la Ununio na Tegeta, Dar es Salaam.

Aidha, katika eneo la Kunduchi, Dar es Salaam vipande ambavyo vilikukatwa ni viganja vya mikono viwili ambavyo kucha zilikuwa zimepakwa rangi, paja moja na kipande cha kalio.

Hukumu hiyo imesomwa leo majira saa 10 jioni na Jaji Awamu Mbagwa wa Mahakama hiyo, baada ya kupitia ushahidi uliyotolewa na mashahidi 25 wa upande wa mashtaka, vielelezo 15, pamoja na utetezi wa mshtakiwa na sheria.

“Ushahidi uliyopo unajitosheleza kuwa mshtakiwa alimuua Ezenia kwa makusudi na mashtaka yamethibitishwa bila kuacha shaka la msingi na upande wa mashtaka dhidi yake,”

 “Abdalah Mussa Miraji ni nakuona unaatia na nina kutia hatiani kwa kosa la kumuua Ezenia Kamana kwa makusudi. Uamuzi huu siyo wa mwisho upande wowote kama haujaridhika unao haki ya kukatia rufaa,”alisema Jaji Mbagwa

Abdalah, anadaiwa Agosti 19, 2024 eneo la Chang’ombe, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, alimuua kwa makusudi Ezenia Kamana.

Mshtakiwa na marehemu walikuwa ni wapenzi uhusiano kwa muda wa miaka minne,mshtakiwa alikuwa anakwenda kutembelea nyumbani kwao Tandika Magorofani akiwa na gari lake. Kutokana na matumizi ya gari la Bluu Mama wa marehemu alimbatiza jina la Mr Bluu.

Marehemu aliondoka nyumbani na kumuacha mama yake, alikuwa anakwenda Kariakoo kwa ajili ya kununua viti vya mgawaha wake nje akiwa anasubiria na mshtakiwa.

Jaji alisema inaonekana wakiwa njiani walitofautiana kauli, iliyosababisha marehemu kushuka katikati ya safari, baada ya muda mshtakiwa alimpigia simu kwamba amfuate maduka mawili Chang’ombe.

Kwa mujibu wa maelezo ya ungamo, chanzo cha ugomvi ni maneno ya marehemu, alimuomba mshtakiwa Sh 100,000 na akamueleza kwaba kwa siku hiyo hakuwa nayo fedha hiyo.

Mshtakiwa alimkumbusha fedha aliyompa kabla ya hapo, Ezenia akamueleza kwamba atairejesha fedha hiyo kwa sababu ni kiasi kidogo ndipo alipokashirishwa na jibu hilo akaamua kuchukua kisu alichokichukua chini ya kiti cha gari.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa hakufikiria kumpeleka hospitali lakini alikaa nae kwenye gari hadi umauti kwa sababu kulikuwa kweupe, aliamua kuendesha gari hadi nyumbani kwake Sinza, alimuingiza nyumbani kwake kwenye chumba chake cha mazoezi.

Alimkatakata vipande na kumuweka kwenye mifuko ya salfeti na kusambaza vipande hivyo sehemu tofauti. Katika juhudi za kumtafuta Marehemu Mr Bluu alikuwa akipigiwa simu hapokei.

Leave a Comment