×

Familia Yatangaza Ratiba ya Mazishi ya Ashlee Jenae, Kuagwa Jumatatu Marekani

Influencer wa mtandaoni Ashly Robinson, maarufu kama Ashlee Jenae enzi za uhai wake.

KIFO cha influencer wa mtandaoni Ashly Robinson, maarufu kama Ashlee Jenae, kimeendelea kuibua maswali huku familia ikitangaza ratiba ya mazishi yake nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanafamilia wa karibu, mwili wa Ashlee unatarajiwa kuagwa kwa siku mbili mfululizo, Jumatatu na Jumanne, kabla ya kufanyika kwa ibada rasmi ya mazishi katika jimbo la New Jersey.

Ashlee alipoteza maisha yake wiki chache baada ya kuwasili Zanzibar kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Aprili 5, 2026 ambapo alimposwa na mchumba wake Joseph McCann, tukio lililovutia hisia kubwa mtandaoni.

Ashlee Jenae enzi za uhai akiwa na mchumba wake Joseph McCann.

Hata hivyo, furaha hiyo iligeuka majonzi kufuatia kifo chake ambacho bado kimezungukwa na sintofahamu. Polisi wa Zanzibar walieleza kuwa kifo hicho kilihusishwa na jaribio la kujiua, lakini uchunguzi unaendelea na mamlaka hazijatoa taarifa kamili ya mwisho.

Ripoti za vyombo vya habari zilidai kuwa mwili wa Ashlee ulirejeshwa Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita, ingawa mamlaka za Zanzibar hazijathibitisha rasmi taarifa hizo.

Haijafahamika pia iwapo Joseph McCann bado yupo Zanzibar, ambapo pasipoti yake iliripotiwa kuzuiliwa na polisi wakati wa awali wa uchunguzi. Hadi sasa, hajatoa kauli yoyote ya hadharani kuhusu kifo cha mchumba wake.

Leave a Comment