
Audi wamezindua rasmi SUV mpya ya umeme inayojulikana kama AUDI E7X, ikiwa ni toleo lililobuniwa mahsusi kwa soko la China.
Gari hilo limewasilishwa kwenye maonesho ya magari ya ‘Beijing Auto Show’ na ni matokeo ya ushirikiano kati ya Audi na SAIC Motor.
E7X ni SUV kubwa ya umeme yenye urefu wa zaidi ya mita tano, ikilinganishwa kwa ukubwa na Range Rover.
E7X itapatikana katika matoleo mawili: Moja ikiwa na nguvu ya takribani farasi 402 (rear-wheel drive) na nyingine yenye nguvu hadi farasi 671 ikiwa na mfumo wa quattro all-wheel drive system. Toleo lenye nguvu zaidi linaweza kutoka 0 hadi 100 km/h kwa sekunde 3.9.

Kwa upande wa teknolojia, gari hili lina mfumo wa 900-volt unaoruhusu kuchaji haraka kutoka asilimia 10 hadi 80 ndani ya dakika 13. Betri zitakuwa na uwezo wa 100kWh au 109kWh, zikiwa na uwezo wa kusafiri hadi kilomita 750 (CLTC).

Ndani, E7X imejaa teknolojia ya kisasa ikiwemo skrini ya panoramic ya inchi 27 mbele, skrini ya nyuma ya inchi 21.4, mfumo wa sauti wa spika 26 kutoka Bose, pamoja na msaidizi wa sauti wa AI. Pia kuna “cinema mode” kwa abiria wa nyuma na chaguo la muundo wa viti vinne kwa ajili ya anasa zaidi.
Kwa nje, muundo wake umeendelea na falsafa ya “urahisi na usahihi,” sawa na ule wa AUDI E5 Sportback. Gari hili linatarajiwa kuanza kuuzwa nchini China kabla ya katikati ya mwaka huu, huku sedan nyingine ya umeme ya AUDI ikitarajiwa kuwasili mwaka ujao.




