
Nissan imerejesha jina maarufu la Nissan Terrano kwa kuzindua concept ya SUV mpya ya plug-in hybrid, inayolenga kushindana na magari makubwa ya off-road kama Toyota Land Cruiser.
Gari hilo limeoneshwa kwenye Beijing Auto Show, likiwa ni sehemu ya mkakati wa Nissan kufufua majina yake ya kihistoria. Kampuni hiyo imethibitisha kuwa toleo la uzalishaji (production version) linatarajiwa kuingia sokoni ndani ya mwaka mmoja.

Terrano mpya imeelezewa kama SUV inayochanganya matumizi ya mijini na uwezo wa safari za nje (off-road). Muundo wake unaonekana kuwa wa kisasa lakini wenye sura ya “boxy” na uimara, ukiwa na ulinzi wa ziada chini ya gari, taa za ziada (auxiliary lights), pamoja na tairi la akiba lililowekwa nyuma.
Pia ina vipengele vinavyoonyesha matumizi ya adventure kama roof rack na michoro ya ramani (topographic details), ishara kuwa inalenga wapenzi wa safari na mazingira magumu.
Kwa sasa, Nissan haijaweka wazi taarifa kamili za mfumo wa nguvu (powertrain), zaidi ya kuthibitisha kuwa itakuwa plug-in hybrid. Ingawa imehakikishwa kuuzwa China, kampuni imesema pia itapatikana katika baadhi ya masoko ya kimataifa.



