×

Maelfu ya Followers Watoweka Instagram, Hiki Ndicho Kinachoendelea

Watumiaji wengi wa Instagram duniani wameamka na kushuhudia idadi ya followers kwenye akaunti zao ikipungua ghafla, jambo lililosababisha mjadala mkubwa mitandaoni kuhusu kile kinachodaiwa kuwa “bot purge” kubwa inayofanywa na Instagram.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali na maoni ya watumiaji kwenye mitandao ya kijamii, Instagram inaonekana kuendelea na operesheni ya kufuta akaunti fake, spam, inactive pamoja na akaunti zisizo halisi ambazo zimekuwa zikiongeza followers kwa njia zisizo za kawaida.

Baadhi ya watengeneza maudhui wakubwa, influencers pamoja na pages maarufu duniani wameripoti kupoteza maelfu hadi mamilioni ya wafuasi (followers) ndani ya muda mfupi. Hali hiyo imewakumbusha wengi matukio ya miaka iliyopita ambapo Instagram ilifanya usafishaji kama huo uliowaathiri hata mastaa na watu maarufu duniani.

Ingawa baadhi ya watumiaji wameonyesha wasiwasi kutokana na kushuka kwa idadi ya followers, wengine wanaamini hatua hiyo inaweza kusaidia kuboresha engagement kwa kuondoa followers fake na shughuli zisizo halisi kwenye platform hiyo.

Hadi sasa, kampuni ya Meta ambayo inamiliki Instagram haijatoa taarifa rasmi kuthibitisha operesheni hiyo, lakini historia inaonyesha kuwa Instagram huwa mara kwa mara inachukua hatua dhidi ya akaunti zinazokiuka sera za matumizi ya platform hiyo.

Watumiaji wengi sasa wanaendelea kufuatilia kama idadi ya followers itaendelea kupungua katika siku zijazo huku wengine wakieleza kuwa wanapendelea kuwa na audience halisi kuliko followers wengi wasiohusika na maudhui yao.

Leave a Comment